SIMBA YALAMBA SUKARI YA MTIBWA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, ameipatia ushindi wa timu hiyo baada ya kuifungia bao la pekee dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar er Salaam.
Okwi aliweka kimiani bao hilo katika  dakika 34  alipoicheza vema pasi ya Uhuru Seleman na kufanya Simba kuendelea kuongoza usukani wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 18, huku nafasi ya pili ikisdhikiliwa na Azam yenye pointi 14..

Comments