SIMBA YAAPA KUWAVUA MAGWANDA MAAFANDE WA POLISI DOM KESHO

SIMBA imeapa kuwaadhiri maafande wa Polisi Dodoma kupitia mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania Bara,utakaopigwa kesho kwenye dimba la Azam lililoko Chamazi Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mabingwa hao wa ngao ya jamii wamejipanga kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ili kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa ligi hiyo.
Simba itashuka dimbani ikiwa na nguvu zaidi kufuatia kushuka dimbvani kwa washambuliaji wake wa  Kimataifa, Felix Sunzu wa Zambia  aliyekuwa akitumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu na Emmanuel Okwi ambaye alikuwa Maputo, Msumbiji na timu ya Taifa ya Uganda iliyokuwa ikishiriki michuano ya All Africa Games (AAG).

Comments