SIMBA v MTIBWA SH.5,000

Mechi namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mtibwa Sugar itachezwa Jumapili (Septemba 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. katika mechi hiyo vitakuwa ifuatavyo; viti vya kijani na bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP B na C sh. 15,000 wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Mauzo ya tiketi yatafanyika siku ya mchezo kwenye magari mbalimbali yatakayokuwa yameegeshwa nje ya Uwanja wa Taifa.
Uwanja wa Taifa pia utakuwa mwenyeji wa mechi nyingine ya ligi hiyo kati ya Yanga na Coastal Union. Mechi hiyo itachezwa Jumatano (Septemba 28 mwaka huu).

Comments