SIMBA CHUPUCHUPU MWANZA, SUNZU AKIMBIZWA HOSPITALI

SIMBA almanusura ilale Mwanza baada ya kulazimisha sare ya mabao 3-3 na Toto African ya Mwanza.
Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la CCM Kirumba, Mwanza ilikuwa na upinzani mkali ambapo Mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma alimtoa kwa kadi nyekundu Philemon Mwandesile ambaye alimchezea rafu mchezaji wa Simba.

Mabao ya Simba yalifungwa na Mzambia Felix Sunzu ambaye alifunga mawili huku Patrick Mafisango akifunga moja, huku yale ya Toto yalifunghwa na Mnigeria Dalington Enyima,  Mohammed Soud na Iddi Mobby.
Aidha, katika mchezo huo Sunzu aliumia baada ya kugongana na mchezaji wa Toto na hivyo kulazimika kukimbizwa hospitali.
Licha ya sare hiyo, Simba imeendelea kukaa kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 15, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 14 na Mtibwa inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 11.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHSeptember 21, 2011 at 9:56 PM

    SHOSTI NAWEWE MBONA UNATUCHANGANYA UNAJUA SISI WENGINE TUNAKUTEGEMEA WEWE TU HATUNA PAHALA PENGINE PA KUYAJUA HAYA!UMESEMA SARE YA 3-3,BAADAE UNASEMA HUYO MZAMBIA WA SIMBA KAPIGA TATU PEKE YAKE,NA HUYO MAFISANGO KAPIGA MOJA KWA UPANDE WA WANYAMA,SASA MATOKEO NI SIMBA 4 TOTO 3 AU HILO LA MAFISANGO LILIKATALIWA?

    MDAU WA YANGA BOMBA,USA

    ReplyDelete
  2. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHSeptember 21, 2011 at 9:57 PM

    HALAFU HIVI KWANINI WANYAMA WANAPATAGA TABU SANA NA HAO WANA?

    ReplyDelete

Post a Comment