NYOTA SITA WATAKAOPATA MAFUNZO TOKA MANCHESTER UNITED WAPATIKANA


Wachezaji sita bora waliochaguliwa katika michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, wakiwa na vyeti vyao baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi, katika kilele cha michuano hiyo, jana kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Wachezaji hao watashiriki kliniki ya Manchester United itakayofanyika Uwanja wa Taifa kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 2, mwaka huu.
Nyota sita waliochaguliwa kutoka Tanzania ni pamoja na Dennis Richard, Seleman Mbovu (kutoka Dar es Salaam), Samir Omar kutoka Mwanza, Charles John, Graham Naftali na Kassim Jungu wote kutoka Morogoro.

Wachezaji wengine watatoka Kenya, Siera Leon na Malawi.

Comments