NEYMAR: REAL, BARCA WOTE WANANITAKA

MCHEZAJI nyota wa Santos, Neymar amekiri kuwa timu za Real Madrid na Barcelona, zote kwa nyakati tofauti zilimtaka na bado zinaendelea kuwania saini yake. Neymar alithibitisha kuwa timu zote mbili, zilikuwa zinapigana kumbo kwa ajili ya kumsainisha lakini alishindwa kufikia nazo makubaliano kutokana na sababu kadhaa.
“Real Madrid na Barcelona zilikuja kwangu na kuanzisha mazungumzo, hili naweza kuthibitisha kabisa, lakini sijaingia nazo mkataba wa aina yoyote ule,” alisema.
Alisema kufuatwa na timu hizo mbili ni jambo la kufurahisha kwake, kwani ni moja kati ya timu zinazoheshimika na zinazokubalika mno.
Baba wa Neymar, hivi karibuni alikiri mwanawe anataka kutua moja kati ya timu hizo mara baada ya msimu wa usajili Ulaya kuanza.

Comments