MWANAMUZIKI KASALOO KYANGA AFARIKI DUNIA

MWANAMUZIKI  siku nyingi  Kasaloo Kyanga ambaye  ni pacha wa  mwanamuziki Kyanga Songa amefariki dunia  leo katika Hospitali ya Mwananyamala Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Akithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo, mmoja ya wakurugenzi wa bendi ya Njenje ambaye aliwahi kufanya kazi na marehemu wakiwa bendi Tuncut Almas, John Kitime, alisema, Kyanga mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) alifariki baada ya kuugua.
 Kyanga aliingia nchini mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kutua bendi ya Super Matimila, kabla ya bade kujiunga na Orchestra Tomatoma na baadae Marquis De Zaire na Tuncut Almasi iliyokuwa na maskani ya Mkoani Iringa.
 Akiwa na Marquis alifanikiwa kutunga na kuimba nyimbo kadhaa na wimbo uliompa umaarufu ni ‘Kalubandika’ kabla ya baadae kuitosa bendi hiyo na kuwika na Tuncut kwa nyimbo kama ‘Masafa Marefu’, ‘Nimemkaribisha Nyoka’, ‘Kashasha’ na nyinginezo.

Marehemu ameacha mjane na watoto sita ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho katika makaburi ya Sinza.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHSeptember 10, 2011 at 5:30 PM

    "Ninakwenda safari...safari yenyewe ya masafa marefu...najua hapa unabaki watasema mengi..pia wabaya wetu mama watafurahi"

    "Tunza watoto mama nitarudi..tutaonana kwa mapenzi ya mungu..."

    R.I.P. Brother KASALOO KYANGA,machozi yamegubika kope za macho yangu,simanzi moyoni,mbele yetu nyuma yako,najua mengi yatasemwa sana juu ya kifo chako lakini mola ndie anaejua sababu ya kifo chako

    mdau yanga bomba,U.S.A.

    ReplyDelete

Post a Comment