MTIBWA YAIKALIA NYUMA SIMBA SC

TIMU ya JKT Ruvu na Toto African ya Mwanza, zimetoka suluhu katika mchezo wao wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mchezo huo ulichezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Kwa matokeo hayo, JKT Ruvu wamejikuta wakishuka hadi nafasi ya tatu kutoka nafasi ya pili baada ya kuzidiwa na Mtibwa Sugar, ambao wana pointi 11, huku JKT wakiwa na pointi 10.
Mchezo ulianza kwa timu zote mbili kusomana, huku kila moja ikifanya mashambulizi ya kushtukiza.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko kwa wachezaji wake, timu zote zilikuwa zikishambuliana, dakika ya 64 JKT Ruvu itabidi wajilaumu baada ya kukosa bao la wazi kupitia kwa mchezaji wao, Hussein Bunu, ambaye alibaki yeye na kipa na kupiga mpira wa kichwa uliopaa juu ya lango la Toto na kutoka nje.
Mchezo huo ulionekana kuwa mgumu, kwani kila timu ilikuwa ikijitahidi kutafuta mabao, lakini zikaishia kutoka suluhu, hadi mpira unamalizika timu hizo hazikufungana.
Toto Africa: Maganga Seif, John Bosco, Philemon Mwendesile, Laban Kambole, Ladslaus Mbogo, Peter Mutabazi/Castor Mumbala, Bakar Kigodeko, Mohammed Soud, Mwita Kemaronge, Iddy Mobby na Phabian James.
Vikosi JKT Ruvu: Hamis Nyangalio, Hassan Kukutwa, Stanley Nkomola, Damas Makwaya, Shaibu Nayopa, Jimmy, Shoji, Sostenes Manyasi, Rajabu Chau, Hussein Bunu, Nashon Naftari na Emmanuel Lenjechele/Haruna John.
Katika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, timu ya Mtibwa Sugar imeifunga Villa Squad mabao 2-0, wafungaji wake wakiwa ni Thomas Morris aliyepiga shuti kali hadi kutoboa nyavu na Said Rashid aliyeunganisha krosi ya Masoud Ally.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar wamepanda hadi nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi 11, huku Villa wakiendelea kusota nafasi ya pili kutoka mwisho kwa kuwa na pointi nne.
Katika Uwanja wa Mlandizi, Pwani, Ruvu Shooting wameifunga Coastal Union mabao 2-1. Mabao ya Ruvu yamefungwa na Ayoub Kipara dakika ya 16 na Seif Abdallah amefunga dakika ya 19. Bao la Coastal limefungwa dakika ya 38 na Aziz Gilla.

Comments

  1. EEH MTIBWA YAIKALIA "NYUMA" SIMBA TENA?!AAH HAYA BWANA HONGERA ZAO

    ReplyDelete

Post a Comment