MTIBWA SUGAR, MORO UNITED ZABANWA



TIMU ya soka ya Moro United  na Ruvu Shooting zimetoshana nguvu katika ligi kuu soka Tanzania Bara  ya 2-2.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Chamazi, bao la Moro liliwekwa kimiani na Godfrey Wambura. hivyo, JKT walisawazisha kupitia kwa Hussein Bunu huku Gaudance Mwaikimba aliifyngia Moro bao la pili kabla ya Alhaj Zege.
Aidha, mechi nyingine iliyopigwa kwenye dimba la Jamhuri mjini Dodoma, Polisi Dodoma ilitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar.
Kutoka  Kagera,  JKT Oljoro imeifunga  Kagera Sugar kwenye uwanja wake wa nyumbani, Kaitaba baada ya kuifunga mabao 2-0.Oljoro iliuanza mchezo huo kwa kasi mabao yote yalifungwa na Amir Omar, huku lile la kufutia machozi la Kagera likifungwa na Themi Felix.
Ruvu Shooting ya Pwani imeiadhibu African Lyon 2-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Magunia uliopo Mlandizi Pwani.
Mabao ya Shootung yalifungwa na Kassim Linde na Abrahman Abdallahman.

Comments