MOROGORO YATWAA UBINGWA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS

Wachezaji wa timu ya Morogoro, wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam Jumamosi, Septemba 24.


Mwamuzi Bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Baraka Rashid akiwa na tuzo yake baada ya kukabidhiwa katika kilele cha michuano hiyo, Jumamosi Septemba 24, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonald Thadeo (kulia), akimkabidhi nahodha wa timu ya kombaini ya vijana wa sekondari za Mkoa wa Morogoro. Charles John, kombe la ubingwa wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, katika kilele cha michuano hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.Katika fainali hiyo Morogoro iliyoongoza kwa pointi ilitoka sare ya bao 1-1 na Dar es Salaam.

 Golikipa Bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Denis Richard wa Mkoa wa Dar es Salaam, akikabidhiwa zawadi ya kikombe na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jane Matimbe katika kilele cha michuano hiyo, jana kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.Fainali za michuano hiyo ilishirikisha timu nne za mikoa ya Morogoro, Iringa, Mwanza na Dar es Salaam.





Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Rahma Mwapachu (kushoto), akimkabidhi zawadi ya kikombe, mchezaji bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Samil Omar wa timu ya Mkoa wa Mwanza,katika kilele cha michuano hiyo, Jumamosi Septemba 24, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu
Timu kombaini ya Mkoa wa Morogoro Jumamosi ilitangazwa bingwa mpya wa michuano ya Airtel Rising Stars 2011 baada ya kwenda sare ya 1-1 na timu ya Dars es Salaam katika mchezo wa mwisho wa michuano hiyo iliyokuwa inachezwa kwa mtindo wa ligi. Timu zingine ambazo zilikshiriki ni kutoka Mwanza na Iringa. Mororogo walitwaa ubingwa huo baada kucheza michezo mitatu ambapo waliweza kushinda miwili na kwenda sare mmoja. Mwanza walikuwa washindi wa pili baada ya kushinda michezo miwili na kupoteza mmoja. Dar es Salaam walipata nafasi ya tatu baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoka sare moja na kupoteza mchezo mmoja. Iringa ndio ilikuwa timu ya mwisho baada ya kupoteza michezo yake yote.
Baada ya kutangazwa bingwa, Morogoro walipata medali ya dhahabu pamoja na vitabu vyenye thamani ya Tshs1m/- (Milioni moja) kutoka kwa wadhamini Airtel Tanzania. Mwanza walipata medali ya shaba na vitabu vyenye thamani ya Tshs500,000/- (laki tano)


Mchezaji bora alikuwa ni Samir Omar kutoka Mwanza huku Ibrahim Hussein akiibuka mfugaji bora. Dennis Richard aliibuka kipa bora na Baraka Rashid akiibuka mwamuzi bora.


Michuano ya Airtel Rising Stars ilizinduliwa hapa nchini mnamo mwezi Juni mwaka, huku yakiwa na madhumuni ya kutafuta wachezaji bora sita wenye umri chini ya miaka 17 ili wajiunge na kambi maalum ya soka ambayo itakuwa hapa nchini chini ya waalimu wa soka kutoka klabu ya Manchester United. Kwa mantiki hiyo, wachezaji waliochanguliwa ni Dennis Richard, Seleman Mbovu (kutoka Dar es Salaam), Samir Omar (Mwanza), Charles John, Graham Naftali na Kassim Jungu( Morogoro)


Katika hatua nyingine, Meneja Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania aliwapongeza wachezaji waliochanguliwa na kuwataka waongeze bidii kwa mafanikio zaidi. Aliyasema hayo wakati wa hotuba ya kufunga michuanoi hiyo. Naye Mkurugenzi wa Michezo nchini Leonald Thadeo ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwata vijana kuwa mabalozi wanzuri wa nchi yetu na kuwataka wale ambao walishiriki lakini hawakuchanguliwa kutokata tama na waendelee na mazoezi zaid. Pia aliipongeza kampuni ya Airtel Tanzani kwa kuamua kuwekeza kwenye sekta ya michezo.

Comments