MASHUJAA MUSICA WAJIPANGA

BENDI ya muziki wa dansi nchini, Mashujaa Musica imejiimarisha zaidi kwa kuongeza wanamuziki wapya sambamba na kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa bendi hiyo, Rahimu Ibrahim, alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kujiweka sawa katika kuelekea uzinduzi wa albamu yao mpya.
Alisema katika kujimaarisha huko wameongeza wasanii watano wapya ambao wameungana na wenzao waliopo kambini kujiandaa na uzinduzi huo.
Aliwataja wanamuziki hao kuwa ni pamoja na Jimmy Adol, Kajo Kajo, Sauti ya Radi, Fred Mazaka na Profa Kariakoo, huku Meneja wake mpya ni Hamis Mahelo.
Alisema kuwa bendi yake inatarajiwa kuzindua albamu yake ya pili hivi yenye nyimbo nane hivi karibuni, ambapo baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na ‘Umeshawahi kwenda kwa Mkweo’, ‘Uchungu wa Moyo’, ‘Hukumu ya mnafiki’ na nyinginezo.

Comments