MASHABIKI WA NDONDI SONGEA KAENI MKAO WA KULA


Kushoto Bondia Saimon Mwakwenda wa Songea akizipiga na  Elieza Mwakipesile wa Njombe, Matokeo Saimon alishinda kwa Pointi, katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Majimaji,Songea. Saiomn anaingia tena ulingoni tarehe 01/10/2011 kuzidunda na Bryan Mwando wa Zimbabwe. Pambano litakuwa la raundi 6 usiokuwa na ubingwa, katika uzani wa Light Middle, kilo 69, ukitanguliwa na mpambano wa wanawake: Zamda Amani wa Songea VS Agness Mtima Ukanena wa Malawi, mchezo huu utakuwa wa raundi nne, uzani wa Walter kilo 66.

Comments