MASAWE MCHEZAJI BORA VPL MWEZI AUGUST

Kiungo wa timu ya Polisi Dodoma, Ibrahim Masawe amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika Ligi Kuu ya Vodacom.Masawe alichaguliwa kwenye mechi namba 4 ya ligi hiyo kati ya timu yake ya Polisi Dodoma na African Lyon iliyochezwa Agosti 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu, Masawe alipata alama 93 ambazo hakuna mchezaji mwingine yeyote aliyefikisha kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Agosti.Kwa kuibuka mchezaji bora wa Agosti, Masawe atazawadiwa kitita cha sh. 600,000 kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Comments