MAHAKAMA YAPIGA STOP MKUTANO WA YANGA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijiji Dar es Salaam, imepiga marufuku mkutano mkuu wa klabu ya Yanga ambao umepangwa kufanyika keshokutwa kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay.
Uamuzi huo umetokana na kuwepo kwa kesi ya msingi namba 98 ya mwaka 2010 ambayo iliisha kwa kuubatilisha uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Lloyd Nchunga (Pichani)kutokana na kuwekwa na katiba batili.
Katika kesi hiyo ambayo hukumu yake ilitoka Julai 1, 2010 na kusisitizwa Agosti 29, mwaka huu, walalamikaji walikuwa wakipinga uhalali wa katiba ya sasa kwa hoja kuwa, katiba halali ni ya mwaka 1968 iliyosajiliwa kwa Kabidhi Wasihi.
Licha ya kubatilishwa kwa uongozi wa Nchunga, hivyo kutakiwa kuondoka madarakani kuipisha Kamati ya Muda chini ya Salim Gereza, bado yupo madarakani na keshokutwa iliitisha Mkutano Mkuu wa Mwaka.

Comments