LIGI SOKA DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 15

Wakati michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inayoshirikisha timu 18 imepangwa kuanza Oktoba 15 mwaka huu timu ambazo hazijakamilisha usajili wa wachezaji zimeongezewa muda hadi Oktoba Mosi mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Septemba 24 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais, Ramadhan Nassib pia imepanga makundi ya ligi hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Oktoba 3-9 mwaka huu majina ya wachezaji walioombewa usajili na timu zote 18 yatabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa TFF kwa ajili ya pingamizi, na Kamati ya Mashindano itakutana Oktoba 10 mwaka huu kwa ajili ya kupitia majina hayo.
Kundi A litakuwa na timu za Mgambo Shooting Stars ya Tanga, Morani ya Manyara, Polisi Dar es Salaam, Temeke United ya Dar es Salaam, Transit Camp ya Dar es Salaam na Burkina Faso ya Morogoro.
Timu zinazounda kundi B ni Majimaji ya Songea, Mbeya City Council, Mlale JKT ya Ruvuma, Polisi Iringa, Small Kids ya Rukwa na Tanzania Prisons ya Mbeya. Kundi C ni 94 KJ ya Dar es Salaam, AFC ya Arusha, Polisi ya Morogoro, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers ya Tabora na Samaria ya Singida.
 

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHSeptember 24, 2011 at 7:07 PM

    NAOMBA UWE UNATUWEKEA UP DATES ZA LIGI HIYO HASA TIMU YA MCC YA MBEYA MAANA INANOLEWA NA RAFIKI YANGU KIPENZI MTU WA WATU JUMA MWAMBUSI,I WANNA KNOW WHAT GOING ON IN HIS CAREER....

    ReplyDelete

Post a Comment