KOCHA wa England, Fabio Capello, ameishutumu Arsenal na kuhoji kama ilifanya busara zaidi kwa kutotilia maana matibabu ya Jack Wilshere na kumruhusu aende mapumzikoni. Capello, alihoji kitendo cha kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kumruhusu mchezaji huyo aende kupumzika kwa muda wa mwezi mmoja, wakati anajua fika alihitaji matibabu.
“Ni kweli aliumia wakati tulipocheza na Uswisi, lakini utashangaa baada ya hapo kocha wake alimruhusu kwenda mapumziko.
“Sio kazi yangu kusema kile kilichotukia, lakini unaweza kujiuliza kwa nini aumie wakati tulipokuwa na Uswisi halafu anapelekwa mapumziko ya mwezi mzima.”
Capello alikuwa akisema hayo kutetea uamuzi wake wa kumchezesha mchezaji huyo katika michuano ya awali ya Euro 2012 hivi karibuni na kudai ulikuwa wa haki.

Comments