KIIZA ATULIUZA MIZUKA YA WANAYANGA BAADA YA KUTUA

MSHAMBULIJI wa kimataifa wa Yanga, Mganda Hamisi Kiiza, amewasili  nchini leo  tayari kwa kuivaa timu ya soka ya Azam Fc mechi itakayopigwa keshokutwa  kwenye dimba la Chamazi.
Kiiza ambaye amekuwa akiwaumiza vichwa viongozi na mashabiki wa Yanga, aliondoka nchini wiki mbili zilizopita kwa ajili ya kuitumikia timu yake ya Taifa ‘The Cranes’ kwenye michuano ya All Africa Games (AAG) nchini Msumbuji kabla ya kutolewa.
Mshambuliaji huyo alipaswa kuripoti katika timu yake ya Yanga tangu juzi, lakini aliamua kubaki jijini Kampala, Uganda, huku akiwa hana mawasilino na viongozi wa Yanga, hali iliyoanza kuwaweka katika hali ya wasiwasi kwamba huenda mchezaji huyo ameanza vituko vyake.

Comments