KIINGILIO YANGA, COASTAL UNION SH.3,000, RUVU SHOOTING YAPIGWA FAINI SH.500,000

Pambano namba 51 la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga na Coastal Union litachezwa Septemba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio vilivyopangwa katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa. VIP C ni sh. 7,000, VIP B ni sh. 10,000 na VIP A itakuwa sh. 15,000.



SHOOTING YAPIGWA FAINI SH. 500,000


Kamati ya Mashindano ya TFF imeipiga faini ya sh. 500,000 timu ya Ruvu Shooting ya Mkoa wa Pwani baada ya kupata kadi sita kwenye mechi namba 40 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Septemba 17 mwaka huu Uwanja wa Mlandizi.
Kwa mujibu wa Kanuni namba 25 (1)(d) ya Ligi Kuu ya Vodacom, timu ambayo wachezaji wake wataoneshwa zaidi ya kadi tano katika mechi moja itatozwa faini ya sh. 500,000.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari

Comments