KESI YA KINA HASSANOO YAPIGWA KALENDA

KESI ya kula njama na kuiba tani 26 za Shaba zenye thamani ya sh milioni 400 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA), Hassan Othman ‘Hassanoo’ na wenzake watatu, jana ilitajwa na kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali, Komanya, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, aliieleza Mahakama kuwa, kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo wanaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine, ili siku hiyo waje kuona kama upelelezi umekamilika au laah.
Ombi hilo lilikubaliwa na Hakimu Nongwa, ambaye aliahirisha hadi Oktoba 12 mwaka huu, ambako Mahakama itakuja kuona kama upelelezi wa shauri hilo kama umekamilika.
Septemba 2 mwaka huu, mawakili wa serikali Andrew Rugarabamu na Aneth Kaganda, walidai mahakamani hapo kuwa, Agosti 26, mwaka huu, maeneo ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam, washitakiwa walikula njama na kuiba shaba hiyo mali ya kampuni ya Liberty Express Ltd ya Dar es Salaam, kwenye gari namba T 821 BCL iliyokuwa inasafirishwa kutoka Zambia.
Wakili Rugarabamu alidai, katika kosa la nne, washitakiwa hao wanadaiwa kupokea tani hizo za shaba kinyume cha sheria, huku wakijua wazi mali hiyo iliibwa.
Mbali na Hassanoo, washtakiwa wengine ni Wambura Kisiroti (32), Dk. Najim Msenga (50), na Salim Shekibula (29), ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu.

Comments

  1. YANGA BOMBA -UHURU BRANCHSeptember 21, 2011 at 6:39 AM

    HAO NDIO WATU WA SIMBA...UPIGAJI KWA KWENDA MBELE,HATA HIVYO NAMPA POLE KWA KUWA TU MTOTO WA KARIAKOO MWENZANGU,OTHERWISE ATAKUTANA NA MKONO WA SHERIA,UZURI NI KWAMBA MWAMBIE UKIMKUTA LEO PALE KT SHOP KWAMBA MAHAKAMANI HAKUNA HAKI BALI KUNA SHERIA TU,HIVYO ASIJALI MAJURA WATU WA MJINI TUNAMUAMINI KWA KESI ZA MAGUMASHI KAMA HIZI,WATASHINDA KESI,ILA MKWANJA LAZIMA UWATOKE

    ReplyDelete

Post a Comment