KAGERA HALI TETE, MECHI TANO HAKUNA USHINDI

MORO United leo imelazimishwa sare ya 2-2 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Chamazi, Mbagala, Dar es Salaam. Kagera sasa imefikisha mechi tano inacheza bila kushinda, maana yake wanaelekea kuzimu. Moro katika mechi zake nne hadi sasa, imeshinda moja, kufungwa moja na kutoka sare mbili.

Comments