JKT RUVYU YAPANDA KILELENI LIGI KUU BARA

MABAO ya Sostenes Manyasi, Rajabu Chau na Emmanuel Lucas leo yameipa ushindi wa 3-0 JKT Ruvu dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam hivyo kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kufikisha pointi tisa.
JKT imeishusha Toto African ya Mwanza iliyokuwa inaongoza ligi hiyo tangu mwanzo na sasa inakabiliwa na changamoto ya kushindana na Simba ambayo kama itaifunga Villa Squad keshokutwa itatimiza pointi tisa.

Comments