JABU AMBADILI MAFTAH STARS

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Jan Poulsen amemuondoa kwenye kikosi chake kinachojiandaa na mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika dhidi ya Morocco,beki wa kushoto Amir Maftah na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Jabu. 
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema jana kweamba, Poulsen amefanya hivyo baada ya daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa kubaini beki huyo bado anasumbuliwa na maumivu. 
Alisema Stars iliyipo kundi D katika mchakato huo, imeingia kambini leo kwenye hoteli ya Chichi iliyoko Kinondoni jijini Dasr es Salaam kwa ajili ya maandalizi mchezo huo utakaochezwa Oktoba 9 mjini Marakkech saa 1.30 jioni.

Comments