FERGUSON AMPONDA SNEDJER

KOCHA wa Manchester United, Alex Ferguson amemponda kiungo Wesley Sneijder na kudai timu yake haikuwa na nia ya kumsajili, kama ilivyodhaniwa na wengi. Awali ilidaiwa kiungo huyo nyota wa Uholanzi, alikuwa karibuni kutua Manchester United kwa ajili ya kuziba pengo la Paul Scholes ambaye aliamua kustaafu. Habari hiyo ikachangiwa zaidi na kauli iliyotolewa na mchezaji huyo ambaye alisema ana nia kubwa ya kucheza soka England, hivyo kuhusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester United.
Lakini Ferguson, ameamua kukata mzizi wa fitina na kudai alikuwa hana nia yoyote ya kumtwaa kwani mchezaji huyo hana uwezo wa kuvaa viatu vya Scholes. “Sneijder wala hakuwa katika mpango wangu wa kuchukua nafasi ya Scholes. Nakubali ni mchezaji mwenye kipaji, lakini huyu hakuwa mawazoni mwangu. Wachezaji pekee kama Xavi na Iniesta (wa Barcelona) ndio unaoweza kuwafananisha na Scholes,” alisema.
Akizungumza na Il Corriere dello Sport jana, Ferguson alisema anasema hilo kwani anajua anachofanya hasa ukichukulia Scholes na Ryan Giggs walikuwa naye toka wakiwa na miaka 13.
Kitu kimoja alichokiri ni kwamba alijaribu kumsajili mkongwe wa AC Milan, Paolo Maldini, lakini jambo hilo lilishindikana.
“Nilijaribu kuzungumza na baba yake, lakini anitazama na kuniona kama kichaa vile na akaniuliza

Comments