CHUO CHA LOUISIANA MAREKANI KUFUNGUA KITUO CHA MICHEZO TANZANIA





UONGOZI wa Chuo cha Louisiana cha Marekani unatarajia kufungua tawi lake hapa nchini ambapo ndani yake kutakuwa na kituo cha kukuza vipaji vya michezo mbalimbali hapa nchini.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni nchini Marekani katika mkutano kati ya uongozi wa Chuo cha Louisiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, alipofanya ziara nchini humo.

Kwa mujibu wa muwezeshaji wa mkutano huo ambaye pia ni mkurugenzi wa timu ya soka ya African Lyon, Mtanzania Rahim Zamunda Kangezi, ambapo Rais Kikwete aliahidi kutoa ekari za ardhi 150 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.
Zamunda alisema kituo hicho kitahusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, kikapu na utengenezaji wa filamu.
Aliongeza kuwa mbali na kituo hicho uongozi huo unatarajia pia kuanzisha shule ya sekondari, sambamba na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juuMsafara wa chuo hicho uliwajumuisha Dk. Randall Esters, Msimamizi wa Elimu na Mwakilishi wa Mahusiano ya Kimataifa na Joseph Cole, Mpangaji wa Mahusiano ya Kirais, ulimshukuru Rais Kikwete kwa kukubali ombi hilo.

Comments