CAF YAINGILIA KATI SAFARI YA STARS CAN 2012 KWA KUPANGA WAKATI MMOJA MECHI KATI YAKE NA MOROCCO NA ILE YA ALGERIA V CAR

Mechi ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu nchini Morocco.
Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo pia ziko kundi D zitacheza tarehe hiyo hiyo na muda huo huo ili kuepuka kupanga matokeo. Mechi hiyo itachezwa jijini Algers.
Waamuzi wa mechi kati ya Stars na Morocco watakuwa Gassama Bakary, Jawo Dickory, Touray Sulayman na Camara Bakary, wote kutoka Gambia. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Zoumaro Gnofame kutoka Togo.

Comments