BOBAN AKEJELIWA TAIFA , MASHABIKI WABWEKA WOW WOW WOW

MASHABIKI wa klabu ya Yanga leo wamemzomea mshambuli wa Simba Haruna Moshi 'Boban' baada ya kukushindwa kuitendea haki pasi ya Ulimboka Mwakingwe baada ya kupiga  shuti kali ambalo lilipaa juu ya lango la Mtibwa Sugar.
Kosa hilo liliperlekea mashabiki hao kuanza  kumzomea wakiita: “Wow wow wow,” wakirejea kitendo cha mchezaji huyo kufukuzwa na mbwa aliyezua tafrani katika mechi baina ya Simba na Toto African ya Mwanza uliopigwa Jumatano na kumalizika kwa sare ya 2-2.
Katika mechi hiyo, Simba iliishinda Mtibwa bao 1-0 baio lililofungwa na Emmanuel Okwi.

Comments