BILICANAS GROUP YADHAMINI SHEAR CHARITY BALL

 MKURUGENZI MTENDAJI WA BILICANAS GROUP DK.LILIAN MBOWE AKIZUNGUMZIA UDHAMINI WAO KATIKA HAFLA YA SHEAR CHARITY BALL ITAKAYOFANYIKA OKTOBA MOSI KWENYE HOTELI YA MOVENPICK
SHEKHA NASSER, MWENYEJI WA TUKIO

KAMPUNI Mama ya Bilicanas Group yenye Kampuni Tanzu za Free Media Limited ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Aishi Protea Hotels, Club Bilicanas na Much More Club imetoa udhamini mnono wa sh. mil 7.5 kwa Kampuni ya Shear Illusions ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya tafrija ya hisani ‘Shear Charity Ball’ iliyopangwa kufanyika Oktoka mosi mwaka huu katika hoteli ya Movenpick Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bilicanas Group Dk. Lilian Mbowe, katika mkutano wa pili wa Shear Charity Ball uliofanyika katika hoteli ya Peacock Jijini Dar es Salaam.
Dk. Mbowe alisema mbali ya fedha hizo pia udhamini mwingine uliotolewa na Bilicanas Group katika tafrija hiyo ni pamoja na kutoa matangazo katika magazeti ya Tanzania Daima na Sayari katika siku maalum kadhalika wameandaa ‘After Party’ itakayofanyika Much More Club mara baada ya tafrija hiyo Oktoba Mosi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Shear Illusions Shekha Nasser alisema kundi la wacheza dansi wa muziki wa miondoko ya Salsa linalofahamika kwa jina la ‘Mutati Dancers’ toka nchini Kenya na Kundi la wasanii kutoka nyumba ya vipaji ya Tanzania House of Talent (THT) watapamba usiku wa tafrija hiyo ya hisani ya Shear.

Comments