BECKHAM AJIANDAA KUWAKIMBIA NIZAR KHALFAN, THIERRY HENRY

Kiungo wa  LA Galaxy ya Marekani, David Beckham akipiga mpira katika mechi dhidi ya Newcastle Jets kwenye Uwanja wa EnergyAustralia mjini Newcastle, Australia. Klabu kadhaa za England zina nia ya kumsajili David Beckham mkataba wake wa kucheza Ligi Kuu ya Marekani (MLS) katia klabu ya Los Angeles Galaxy utakapoisha mwishoni mwa mwaka huu. Tottenham na Queens Park Rangers wamezungumzia wiki hii kuwa na mpango huo wa kumrejesha Ligi Kuu ya England Nahodha huyo wa zamani wa Englandifikapo Januari. Mtanzania Nizar Khalfan anacheza MLS katika klabu ya Vancouver ya Canada, wakati mshambuliahji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry anacheza ligi hiyo katika klabu ya New York Red Bull. 

Comments