AZAM YASHIKWA ARUSHA


Timu ya Azam FC leo wameshindwa kutamba katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid pale walipo alikwa na JKT Oljoro katika mpambano wa ligi kuu ya vodacom na kwisha kwa sare ya goli 1-1.
Katika mchezo huo Azam FC walikuwa wa mwanzo kuandika goli kupitia kwa mshambuliaji wao hatari John Bocco katika dakika ya 40, huku Oljoro wakisawazisha katika kipindi cha pili.
Moderator wa Azam FC facebook page aliwashtumu marefa kuwa ni chachu ya wao kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa leo.
Mchezo mwingine wa ligi kuu ulipigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga na kushuhudia wenyeji Coastal Union wakipokea kichapo toka kwa vijana watabata Moro united.
Moro united walijipatia goli lake la kwanza kupitia kwa Gaudence Mwaikimba kabla ya Coastal kusawazisha goli hii. Na huku beki wa Coastal union akijifunga na kuipa ushindi wa goli 2-1 Moro united.

MSIMAMO WA VPL.
KwenyeMabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (3) 9
2. JKT Ruvu (5) 9
3. Mtibwa Sugar ( 5) 8 4. Moro United (5) 8
5. Toto Africa ( 5) 7
6. JKT Oljoro (5) 6
7. Africa lyon (4) 5
8. Coastal Union (5) 4
9. Villa Squad (4) 4
10 . Kagera Sugar (5) 4
11 . Azam FC ( 3) 4
12 . Polisi Dodoma (4) 3
13 . Ruvu Shooting (4) 3
14 . Yanga SC (3) 2
 

Comments

  1. Twiga star na bayanabanya ni dk ya 36 mabao ni 0-0

    ReplyDelete
  2. HAWA WATOTO WA BAKHRESA NAO WANA MATATIZO GANI?MKWANJA WANAO LAKINI WANASHINDWA KUCHEZA MPIRA WHAT'S WRONG WITH U GUYS MEN,CALM ON PULL UP UR SOX!

    ReplyDelete

Post a Comment