AZAM FC YAZITIMUA SIMBA, YANGA CHAMAZI COMPLEX

UONGOZI wa klabu ya Azam FC ya Dar es laam umeliomba Shirikisho la soka la Tanzania (TFF) kuzihamisha timu za Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikutumia uwanja wao uliopo Chamazi kwa mechi zake za nyumbani.
Msemaji wa Azam Fc Jaffer Idd amesema TFF hawana budi kuzihamishia timu hizo katika dimba la CCM Kirumba, Mwanza kwani dimba la Chamazi lina uwezo wa kuchukua watu 3000 idadi ambayo ni ndogo kwa mechi zinazohusu timu hizo.
Simba na Yanga zilikuwa zikiutumia uwanja wa Taifa kabla ya seriukali kuufunga kwa ajili ya ukarabati na hivyo vigogo hao vikahamia mikoani ambapo Simba ilikwenda Tanga na Yanga ikatimkia Morogoro.
Hata hivyo SDerikali ilikuja ziruhusu tena timu hizo kuutumia Uwanja huo kwa masharti, hivyo TFF kuzihamishia mechi za Simba na Yanga katika dimba la Chamazi.

Comments