ARSENAL WAKALIA GOGO, YAKUBU AWAFANYA MBAYA

ARSENAL bado gonjwa, ndivyo unavyoweza kuwaambia mashabiki wa Gunners ukikutana nao, baada ya jana kupigwa 4-3 na Blackburn Rovers, ambao walijipatia ushindi wa kwanza kwenye ligi hiyo na kumpunguzia jakamoyo kocha Steve Kean. Rovers walitoka nyuma na kuwabana Arsenal kwenye mchezo huo, Uwanja wa Ewood Park.
The Gunners walipata bao la kuongoza kupitia kwa Gervinho dakika ya 10, aliyekuwa umbali wa mita 12, lakini Blackburn ilisawazisha kupitia kwa Yakubu dakika ya 25.
Mikel Arteta aliifungia Arsenal bao la pili dakika ya 34 akiwa umbali wa mita 18, kabla ya Alex Song kujifunga dakika ya 50 na kuwasawazishia wenyeji.
Yakubu alifunga la tatu dakika ya 59, kabla ya Laurent Koscielny naye kujifunga dakika ya 68 na Marouane Chamakh kuifungia la tatu Arsenal dakika ya 85.
Kikosi cha Arsenal jana kilikuwa; Szczesny, Sagna/Djourou dk 53, Mertesacker, Koscielny, Santos, Arteta, Ramsey, Song/Chamakh dk 76, Arshavin/Walcott dk 64, Van Persie na Gervinho.
Blackburn: Robinson, Salgado/Petrovic dk 18, Samba, Givet, Dann, Formica/Vukcevic dk 65, Nzonzi, Lowe, Rochina/Olsson dk 56, Hoilett na Yakubu.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHSeptember 18, 2011 at 7:41 AM

    MTOTO UNA MANENO MABAYA WEWE ETI ARSENAL WAKALIA GOGO!

    ReplyDelete

Post a Comment