AKINA MESSI WAWATANDIKA NIGERIA 3-1

Nyota wa Argentina, Lionel Messi akilalamika uwanjani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa taifa wa Bangabandhu, mjini Dhaka leo. Agentina iliifunga Nigeria 3-1.
ARGENTINA jana iliishindilia Nigeria kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika jana mjini hapa, ambao ulikuwa mkali na wa kuvutia kwa muda wote.

Mabao ya Argentina katika mchezo huo yaliwekwa kimiani na Gonzalo Higuain dakika ya 24 na Angel Fabian Di Maria katika dakika ya 24, huku Uwa Elderson Echiejile akijifunga mnamo dakika ya 65.
Bao la Nigeria katika mchezo huo liliwekwa kimiani na Chinedu Ogbuke Obasi mnamo dakika ya 46, ambaye alifufua matumaini ya timu hiyo kuibana Argentina.
Katika mchezo mwingine uliofanyika London, Brazil iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana ambao nao ulikuwa mkali na wa kuvutia kwa muda wote.

Comments