AJALI YA MV SPICE ISLANDERS YAMGUSA SHIBOLI

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar Ali Ahmed Shiboli (pichani)yupo katika maombolezo makubwa kufuatia kumpoteza mdogo wake katika ajali ya meli ya MV Spice Islandes iliyotokea usiku wa kuamkia jumamosi huko Nungwi, Visiwani Pemba.
Katika ajali hiyo ambayo inakadiriwa kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200, Shiboli alimpoteza mtoto wa mama yake mdogo Ally Rashid.
"Kwa kweli ajali hii imetugusa wengi sana,  lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba mwili wa mdogo wangu ambaye alikuwemo ndani ya meli hiyo haujapatikana mpaka sasa,"Alisema.
"Inasikitisha kwa kweli lakini yote ni mipango ya mwenyezi mungu hivyo kinachotakiwa ni kuwaombea wapumzike kwa amani waliotangulia mbele ya haki...pia tunawaombea nafuu waliopata majeraha kupitia ajali hiyo,"Aliongeza Shiboli.

Comments