'ADEBAYOR' AWASHUSHA THAMANI SUNZU, KIPRE TCHECHE

MSHAMBULIAJI wa Azam FC John Bocco ‘Adebayor’ hadi sasa amewazidi kwa ubora wa ufungaji wa magoli wachezaji wa kimataifa waliosajiliwa kwa mamilioni ya fedha katika klabu mbalimbali hapa nchini.

Katika mechi nane alizocheza, Adebayor amefunga mabao matano hivyo kuongoza mbio za kiatu cha dhahabu, akifuatiwa na Gaudance Mwaikimba wa Moro United amwenye mabao manne na mgeni pekee kwenye ligi hiyo, Patrick Mutesa Mafisango wa Simba ambaye pia ana mabao manne.
Ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Agosti 20, ilitaraji kutawaliwa na washambuliaji wa kigeni waliosajiliwa kutoka nchi mbalimbali akiwemo Mfungaji bora wa michuano ya Chalenji mwaka 2010, Mzambia Felix Sunzu.
Wachezaji wengine wa kimataifa waliosajiliwa na timu zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Haruna Niyonzima, Davies Mwape, Hamis Kiiza, Kenneth Asamoah (Yanga), Gervas Kago,Darlington Enyima wa Toto African, Wahab Yahaya, Kipre Tcheche wa Azam na wengineo.

Comments