YANGA YASEMA KATIBA HAIWARUHUSU KUVAA RANGI NYEKUNDU, YAWATAKA WANACHAMA KUWA NA SUBIRA

YANGA imesema itakuwa ngumu kuvaa jezi mpya zilizotolewa na wadhamini wa ligi kuu ya Vodacom kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kutokana na kwamba katibva yao hairuhusu kuweka rangi nyekundu.


Hiyo inafuatia Vodacom kubadili nembo yake ambapo kwa sasa inarangi nyekundu na nyeupe wakati katiba ya Yanga inawataka kuvaa rangi ya njano na kijani tu.

Aidha Yanga imesema kuwa hawana mkataba wa udhamini na Vodacom bali ni shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hivyo wataendelea kuvaa jezi za mmoja ya wadhamini waol kampunio ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanajaro na si Vodacom.

Katioka hatua nyingine, wamesema kufabnya kwao vibaya katika mechi yao ya kwanza ya ligi kuu soka Tanzania Bara juzi kulichangiwa na Uwanja mmbovu, pia maamuzi mabovu yaliyokuwa yakitolewa na mwamuzi wa mcvhezo huo dhidi yao hali.

Katika mechi hiyo dhidi ya JKT Ruvu, Yanga ililamnbwa bao 1-0, huku wakiwataka wanachama wao kuwa watulivu kwani hata mwaka jana walianza vibaya na mwishowe wakatwaa ubingwa.

Comments