YANGA YAPIGWA 3-1 TENA SUDAN


Beki wa Yanga, Nadir Cannavaro akitafuta mbinu za kuwadhibiti washambuliaji wa El Hilal

YANGA imemaliza ziara yake nchini Sudan kwa kufungwa tena mabao 3-1 na El Hilal ya Sudan usiku huu. Yanga ilikuwa ya kwanza kupata baio kipindi cha kwanza, mfungaji Kenneth Asamoah, lakini kuumia kwa kipa Yaw Berko kulikofanya Said Mohamed akachukue nafasi kuliiponza klabu hiyo kufungwa mabao matatu kipindi cha pili na kulala 3-1. Katika mchezo wa kwanza, Yanga ililala pia 3-1, bao la mabingwa hao wa Bara likitiwa kimiani na Kiiza Hamisi. Yanga inatarajiwa kurejea leo usiku kuendelea na maandalizi ya mechi ya mechi ya Ngao dhidi hya Simba, Agosti 17, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments