YANGA YAONDOKA NA WACHEZAJI WAKE WA STAZ

KADO SAFARINI SUDAN

YANGA leo impuuza agizo la kuwaacha wachezaji wake saba wajiunge na Taifa Stars na kuondoka nao kwenda Sudan, kwa ziara ya mechi mbili za kirafiki ya kwanza ikichezwa leo dhidi ya Al Hilal, inayofundishwa na Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’.

Walioondoka ni Shaaban Kado, Nsajigwa Shadrack, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Chacha Marwa, Godfrey Taifa, Julius Mrope na Juma Seif 'Kijiko' wakiingia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kupanda ndege ya Ethiopia Airlines kuelekea Sudan.
Wachezaji wengine walioondoka jana ni makipa Mghana Yaw Berko, Said Mohammed, mabeki Oscar Joshua, Bakari Mbegu na Abuu Ubwa, viungo ni Julius Mrope, Godfrey Bonny, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’, Rashid ‘Chiddy’ Gumbo na Kigi Makassy, wakati washambuliaji ni Mghana Kenneth Asamoah, Mganda Hamis Kiiza na Jerry Tegete.

Comments