YANGA YAKATAA WACHEZAJI WAKE KUJIUNGA STARS

NAHODHA WA YANGA NA TAIFA STARS NSAJIGWA SHADRACK

WAKATI timu ya ya Tanzania, Taifa Stars ikijiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan, uongozi wa klabu ya Yanga umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwasamehe juu ya wachezaji wake kujiunga na timu hiyo.

Yanga ina wachezaji nane katika kikosi cha Stars kilichoitwa na kocha Jan Poulsen hivi karibuni, ambao ni Shabani Kado, Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub'Canavaro', Chacha Marwa, Julius Mrope, Juma Seif, Nurdin Bakari pamoja na Godfrery Taita.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati wataondoka leo kuelekea Sudan walipopata mwaliko wa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya El Merreikh na Al Halil wiki ijayo michezo itayoingiliana na ile ya timu za taifa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema TFF wanapaswa kuwasamehe kwa hilo kwa sababu klabu hiyo pia inaenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mechi hizo mbili za kirafiki itakazocheza nchini humo.

Comments