YANGA YAINGIWA MCHECHETO, YATIMUA MASHABIKI

SIKU chache zikiwa zimesalia kabla ya mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Yanga kukwaana na mahasimu wao wa jadi Simba, uongozi umeamua kuzuia mashabiki kushuhudia mazoezi ya wachezaji wa timu hiyo.
Yanga imefikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa kocha wao mkuu Sam Timbe kuwapa mazoezi muhimu na wachezaji kuweza kuyapata mafunzo hayo wakiwa katika hali ya utulivu.
Yanga itakwaana na Simba jumatano ijayo katika mechi ya kuwania ngao ya jamii itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Comments