YAMETIMIA, FABREGAS ALIKUWEPO ARSENAL...

CESC Fabregas amemaliza sakata lake la usajili na hatimaye kumwaga wino kwenye mkataba wa miaka mitano wa kuchezea Barcelona. Barcelona ilitoa kitita cha pauni 35 milioni (Sh. 90 bilioni) na kumalizana na Arsenal sasa kazi ikabaki kukaa na Fabregas kuweka sawa mambo ya mshahara.  Fabregas alifikia muafaka na Barcelona jana Jumatatu asubuhi na akapimwa afya yake.  Kiungo huyo alikabidhiwa jezi namba 4 mbele ya mashabiki wa Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp na ikikumbuka ilivyompata kwa mbinde Fabregas, Barca imeweka sharti gumu kwa timu itakayotaka kumsajili kwa sasa.
Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal amewekewa kipengele cha kumfunga cha dau la pauni 175 milioni (Sh. 175 bilioni) kwa timu itakayomtaka.
Fabregas, ambaye alilelewa katika klabu hiyo kabla ya kunyakuliwa na Arsenal mwaka 2003 alisema: "Kwangu mimi ni siku ya pekee kujiunga na Barcelona kwani nimerudi nyumbani."

Comments