WILL SMITH, JADA WAACHANA

MWISHONI mwa mwezi uliopita waliamua kuita waandishi wa habari na kufungua milango, huku wakiwaonyesha nyumba yao mpya iliyopo eneo la Malibu. Walidai kutokana na uwepo wa nyumba hiyo yenye kila kitu, wanaamini penzi lao litadumu zaidi na watakuwa na maisha mazuri zaidi kuliko wengine wote wale. Katika ziara hiyo, walipigwa picha wakiwa na furaha kubwa mioyoni mwao, lakini kumbe mambo yote ni tofauti na walikuwa na mambo mengine katika vichwa vyao.
Sasa imethibitika rasmi nyota wawili waliokuwa wanachukuliwa kama mfano ndani ya Hollywood, Will Smith, 42, na mkewe Jada Pinkett-Smith wameachana rasmi baada ya miaka 13 ya ndoa.
Wawili hao ambao wameishi kwa miaka 13, wamethibtisha kwamba wameamua kufikia mwisho wa maisha yao ya ndoa na kukubaliana kuachana huku wakikataa kutaja sababu.
Will na Jada wana watoto wawili ambao ni Jaden, 13 na Willow, mwenye miaka kumi. Will pia ana mtoto mwingine aitwaye Willard Christopher Smith, ambaye pia anafahamika kwa jina la Trey mwenye miaka 18.

Comments