WENGER: SIJIUZULU NG'O

ARSENE WENGER amesema hatajiuzulu Arsenal pamoja na kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa Manchester United. The Gunners walikung'utwa 8-2 kwenye Uwanja wa Old Trafford leo, lakini Wenger, ambaye anasherehekea miaka 15 kazini mwezi ujao, alisema: "Naamini tuna mapumziko kabla ya mechi ijayo,". kuhusu kujiuzulu, alisema; "Hapana, hapana kabisa."Wenger ameshuhudia Nahodha wake Cesc Fabregas akitimkia Barcelona na Samir Nasri na  Gael Clichy wamejiunga na Manchester City, wakati kocha huyo Mfaransa amewasajili Gervinho na Alex Oxlade-Chamberlain, ingawa mashabiki wa Gunners wanataka sura mpya zaidi.
Lakini Wenger amesistiza kutumia fedha haliwezi kuwa jibu la matatizo ya Arsenal.

Comments