WATATU WALIOWEKA REKODI YA UHAMISHO ENGLAND...

NAMBA 1. Cristiano Ronaldo aliondoka Man United kwa dau la pauni Milioni 80 kwenda Real Madrid mwaka 2009- huyo ndiye anayeongoza katika historia ya soka kuhamishwa kwa dau kubwa akivunja rekodi ya dau la pauni Milioni 53, ambazo Real Madrid ilitoa kumnunua Zinedine Zidane kutoka Juventus mwaka 2001.


NAMBA 2. Fernando Torres aliondoka Liverpool kwenda Chelsea mwaka 2011 kwa dau lililovunja rekodi kwenye Ligi Kuu ya England, pauni Milioni 50, ingawa uhamisho wa Zlatan Ibrahimovic kwenda Barcelona na Kaka kutua Real Madrid mwaka  2009 uligharimu zaidi.



NAMBA 3. Muargentina Sergio Aguero amejiunga na Manchester City kutoka Atletico Madrid mwaka  2011 kwa dau la pauni Milioni 38, dau ambalo sawa na Lazio ilitoa kwa Parma kumnasa Hernan Crespo na Juventus ilitoa kwa Parma kumnunua Gianluigi Buffon mwaka 2000 na 2001.


Comments