WASHIRIKI BSS-SECOND CHANCE KUWASHA MOTO MZALENDO PUB KESHO


 BEATRICE WILLIAM
 BELLA KOMBO
SARAFINA MSHINDO

WASHIRIKI  wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Seach ‘BSS’-Second Chance, kesho  wanatarajiwa kutoa burudani katika Ukumbi wa Mzalendo Pub,imefahamika.
 Washiriki hao watapanda katika jukwaa la ukumbi huo ambao leo hupambwa na usiku uliobatizwa kama ‘Fleva Nite’. 
Msemaji wa Fleva Nite Boniventure Kilosa ‘Dj Venture’, alisema janja kwamba lengo la kuwapandisha jukwaani washiriki hao ni kutoa nafasi ya kuwaburudisha mashabiki watakaojitokeza katika ukumbi huo. 
Alisema, wameshazungumza na waandaaji wa shindano hilo na kwamba shoo hiyo ni sehemu ya utaratibu wa shindano hilo kufanya maonyesho sehemu mbalimbali hadi kufikia hatua ya fainali ya shindano hilo hapo baadaye. 
“Mambo yote yatakwenda kama kawaida tutapiga nyimbo za zamani na za sasa pamoja na washiriki hao wa BSS ‘kukamua’, naamini mashabiki watafurahia ‘shoo’ ya Jumamosi na waje waone mambo ya washiriki hao,” alisema Venture.

Baadhi ya washiriki hao watakaotoa burudani katika ukumbi huo wa Mzalendo Pub hapo kesho ni Marry Lucos, Haji Ramadhani, Beatrice Wiliam, Roger Lucas, Mwapwani Yahaya, Sarafina Mshindo na Bella Kombo

Comments