WASHIRI BSS KUKAMUA MZALENDO PUB J'MOSI

WASHIRIKI wa shindano la kusaka vipaji vya uimbaji la Bongo Star Search (BSS –Second Chance) 2011 , Jumamosi hii wanatarajiwa kufanya onyesho jingine kwenye disko la Fleva Night, katika Ukumbi wa Mzalendo Pub.
Msemaji wa disko hilo linalofanyika kila Jumamosi katika ukumbi huo , Boniventure Kilosa ‘Dj Venture’ alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na maombi ya mashabiki wao kutaka burudani kutoka kwa washiriki hao.
Alisema, mara ya kwanza onyesho hilo lilifana sana hawana budi kupokea maombi ya mashabiki wao kwa kuirejesha kwa mara nyingine burudani hiyo.Dj Venture aliongeza kuwa wamefanya mazungumzo na wahusika wa BSS ambao wamekubali hivyo Jumamosi hii itakuwa nafasi nyingine kwa wale waliotoa maombi hayo na kushindwa kuhudhuria onyesho la kwanza kupata burudani kutoka kwa washiriki hao.
Shindano hilo linaandaliwa na kampuni ya Benchmark Production inaandaa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi septemba mwaka huu ambapo tayari washiriki waliotinga hatua ya kumi bora ya shindano hilo.

Washiriki hao ni pamoja Rogers Lucas, Bella Kombo, Chibi Dayo, Sarafina Mshindo, Hajji Ramadhan, Mary Lucos, Waziri Salum, Beatrice William na Iman Lissu.

Comments