WAREMBO MISS TANZANIA WAZURU MONDULI


 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Regina Lowasa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha Namelok Sokoine wakicheza mziki wa Kwaito na Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha warembo hao katika mji wa Monduli juzi mkoani Arusha. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo

Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa wamevalia vazi maalum livaliwalo na wanawake wa jamii ya Kimasaai wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.

Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipakua chakula wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika mji wa Monduli jana. Tafrija hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa.

 Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao baada ya kukaribishwa katika mji wa Monduli jana katika tafrija iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine akimshika mkono mmoja wa washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania baada ya kuvishwa mgolole wa kimasai na dada wa Mbunge wa Monduli, Kalaine Lowasa (wapili kushoto) jana baada ya kuwasili Monduli. Kushoto ni Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga.

Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiangalia nyoka aina ya chatu wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.

 Blessing Ngowi, Mshiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, akiwa amejivisha nyoka shingoni huku wenzake wakimwangalia wakati warembo hao na wenzao walipotembelea eneo la Snake Park mkoani Arusha jana. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao baada ya kukaribishwa katika mji wa Monduli jana katika tafrija iliyoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine na dada wa Mbunge wa Monduli Kalaine Lowasa

Comments