VIONGOZI KIFA WAKABIDHIWA OFISI NA DENI LA SHILINGI 800,000


VIONGOZI wapya wa Chama cha Soka cha Wilaya ya Kinondoni (KIFA) wamekabidhiwa rasmi ofisi huku kukiwa na deni linalofikia shilingi 800,000, huku kiasi kilichobaki katika akaunti kikiwa shilingi 33,000.
Aliyekuwa katibu mkuu wa Kifa Frank Mchaki ndiye aliyekabidhi ofisi kwa uongozi mpya wa Kifa chini ya Mwenyekiti wake Michael Lupiana.
Katibu Mkuu mpya wa Kifa Isaac Mazwile (Pichani) alisema katika deni hilo fedha nyingi zinadaiwa na waamuzi ambao walikuwa wanachezesha ligi  ya Taifa ngazi ya Wilaya.
 Alisema chama hicho pia kinadai  kiasi cha shilingi mil.1.3 kama malipo ya pango kwa watu ambao wamepanga kwenye maduka ambayo majengo yake yanamilikiwa na chama hicho.
 Mazwile aliobngeza kuwa mara baada ya kukabidhiwa ofisi hizo wataangalia uwezekano wa kupata ofisi nyingine kutokana na ukweli kwamba ofisi hizo hazina hadhi , huku wakipanga kwenda kwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuangalia uwezekano wa kupata ofisi katika manispaa hiyo.
 Aidha, Katibu huyo aliongeza kuwa uongozi huo mpya unatarajiwa kuanza kushughulikia changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiikabili Wilaya hiyo, hivyo amewaomba wadau kuwa na subira.

Comments