ULAYA KWA UFUPI...

Manchester City 4 Swansea 0

SERGIO AGUERO amehakikisha kwamba Carlos Tevez anaweza asiwe na umuhimu wowote, baada ya juzi usiku kufanikiwa kupachika wavuni mabao mawili wakati Manchester City ilipokwaana na Swansea. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu, Man City ilishinda kwa mabao 4-0.

Meireles atakiwa Chelsea
TIMU ya Chelsea inaonekana inataka kujiimarisha zaidi kwani kwa sasa inataka kumtwaa kiungo wa Liverpool, Raul Meireles. Hayo yamekuja huku Liverpool, ikiwa ipo tayari kumuuza mchezaji huyo.

Walcott amchefua Capello
MCHEZAJI kinda wa England, Theo Walcott amemchefua kocha wa timu hiyo ya taifa, Fabio Capello kuhusu kitabu chake kipya alichotoa ambapo amemshutumu kwa mambo kadhaa. Capello amesikitishwa na kitendo cha Walcott kumshutumu bila sababu za msingi.

Gallas kukaa benchi
BEKI mahiri William Gallas, 33, anaweza kuzikosa mechi za awali za ‘Europa League’ kutokana na kuwa majeruhi. Kwa sasa Ledley King ndiye amejumuishwa katika michezo hiyo ya awali, huku Gallas akitazamwa kwanza afya yake.

Kean katika shinikizo
KOCHA wa Blackburn, Steve Kean ameingia katika shinikizo kubwa kutoka kwa matajiri wake baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa. Mhindi anayeimiliki timu hiyo, Venky anaamini kosa hilo ni la kujitakia zaidi.

Villas-Boas amn’ang’ania Modric
CHELSEA imerudi tena katika mbio zake za kumuwania mchezaji Luka Modric na safari hii imeshika mkononi kiasi cha pauni milioni 30. Kocha Andre Villas-Boas, anaamini kutua kwa Modric, kutamaliza tatizo la kiungo katika timu hiyo.

Enrique amfagilia Carroll
MCHEZAJI Jose Enrique amewaonya mabeki wa timu za Ligi Kuu, wakae mkao wa kutiwa simanzi na Andy Carroll, kwani kwa sasa anataka kurudi katika makali yake. Liverpool ilimsajili Carroll kwa kiasi cha pauni milioni 33.

Odemwingie mambo bado
TIMU ya West Bromwich imedai kama kuna timu inamtaka mshambuliaji wake Peter Odemwingie ni lazima itoe kiasi cha pauni milioni 8 na si vinginevyo. Wigan ilikuwa tayari kutoa nusu ya fedha hizo, lakini ikakataliwa kumtwaa.

Barton akwepa adhabu
JOEY BARTON amekwepa kifungo chochote kutoka kwa Chama cha Soka (FA), kutokana na kusababisha mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho atolewe nje ya uwanja wakati timu zao zilipokwaana. Newcastle ilikwaana na Arsenal mwishoni mwa wiki katika mchezo waLigi Kuu.

Chris Samba atakiwa
MCHEZAJI tegemeo wa Blackburn, Chris Samba amekiri kwamba kwa sasa anawaniwa na timu za Arsenal na Tottenham zinazomtaka atue hapo. Kocha wa Blackburn, Steve Kean amekiri mchezaji huyo kutakiwa na timu kadhaa.

Shevchenko majeruhi matupu
MSHAMBULIAJI mkongwe, Andriy Shevchenko ambaye kwa sasa anaichezea Dynamo Kiev, ni majeruhi na kuna uwezekano akaa nje ya uwanja kwa muda mrefu. Hiyo ni baada ya pia kudaiwa anasumbuliwa pia na tatizo la kichwa.

Toure apiga jalamba
KOLO Toure amerejea tena katika mazoezi ndani ya Manchester City, ikiwa siku chache kabla ya adhabu yake ya kufungiwa kwa miezi sita kumalizika Septemba 2, mwaka huu. Kolo alifungiwa kutokana na kutumia vidonge vilivyopigwa marufuku.

%%%



Comments