TWANGA PEPETA KULA IDD PILI TCC CLUB, CHANG'OMBE

Bendi maarufu nchini African Stars `Twanga Pepeta, itatumbuiza katika onyesho maalum ijulikanalo kama ‘Konyagi Iddi Pili Show’ ambalo limepamgwa kufanyika kwenye ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe, Temeke siku ya Iddi Pili. Mratibu wa onyesho hilo , Joseph Kapinga, amesema hilo la pekee la aina yake limeandaliwa na Bob Entertainment chini ya udhaminbi wa kinywaji cha Konyagi.

Kapinga alisema burudani hiyo ni maalum kwa ajili ya kusindiza sherehe ya Iddi Pili.

Naye mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, amesema kuwa onyesho hilo litatumika kutangaza albamu yao mpya inayotarajiwa kutambulishwa rasmi baadaye mwaka huu.

Nyimbo zilizomo kwenye albamu mpya ya Twanga Pepeta ni pamoja na Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na Penzi la shemeji.
Kapinga alisema kuwa onyesho la TCC pia litatumika kumtambulisha Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis ambaye amejiunga na bendi hiyo kuchukua nafasi ya mnenguaji Aisha Madinda aliyetimkia katika Bendi ya Extra Bongo.

Comments