TIP TOP CONNECTION KULA IDD DODOMA

KUNDI la muziki wa bongo fleva, Tip Top Connection litapoga shoo kali kwa wakazi wa Dodoma siku ya sikukuu ya Idd Mosi.
Meneja wa kundi hilo Babu Tale (Pichani)amesma kikosi kizima cha wakali hao wenye maskani yake Manzese, Dar es Salaam amesema mashabiki wa huko wakae mkao wa kula.
Kundi la Tip Top Connection linaundwa na vichwa vikali kama Madee, Tundaman, Cassim Mganga, Desso, Richard na Dogo Janja.

Comments